Jeremiah 22:24-27

24 a“Hakika kama niishivyo,” asema Bwana, “hata kama wewe, Yekonia
Yekonia au Konia ni jina jingine la Yehoyakini.
mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, ungekuwa pete yangu ya muhuri katika mkono wangu wa kuume, bado ningekungʼoa hapo.
25 cNitakutia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wako, wale unaowaogopa, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na kwa Wakaldayo. 26 dNitakutupa mbali wewe na mama aliyekuzaa mwende katika nchi nyingine, ambayo hakuna hata mmoja wenu aliyezaliwa huko, nanyi mtafia huko. 27Kamwe hamtarudi katika nchi mliyotamani kuirudia.”

Copyright information for SwhNEN